Ni kipi kilichowekwa katika Shari´ah kufanya wakati wa kumfukia maiti na udongo?

Swali: Ni kipi kilichowekwa katika Shari´ah pindi linapofukiwa kaburi? Imewekwa katika Shari´ah kusema:

مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَى

“Kutoka humo [ardhini] Tumekuumbeni na katika hiyo [ardhi] tutakurudisheni na kutoka humo tutakutoeni kwa mara nyingine.” (20:55)

Jibu: Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa imesuniwa kurusha udongo mara tatu kwenye kaburi. Hata hivyo hakuna Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayotegemewa ya kwamba mtu aseme:

مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَى

“Kutoka humo [ardhini] Tumekuumbeni na katika hiyo [ardhi] tutakurudisheni na kutoka humo tutakutoeni kwa mara nyingine.”

Kilichosuniwa baada ya mazishi ni kufuata yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyoamrisha. Alipokuwa anamaliza kuzika alikuwa akisimama karibu na kaburi lake na kusema:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti. Hakika hivi sasa ataulizwa.”[1]

Muombeeni Allaah amthibitishe na amthibitishe kisha ondokeni.

[1] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/185)
  • Imechapishwa: 24/08/2021