Ni ipi hukumu ya sanduku linalowekwa kwenye jeneza la mwanamke?

Swali: Ni yapi maoni yako juu ya sanduku linalowekwa juu ya jeneza la mwanamke kwa ajili ya kumsitiri? Je, mwanamke amekatazwa kuonekana sawa akiwa hai au maiti? Je, sanduku hili ni Sunnah? Kama ni Sunnah ni kwa nini isihuishwe na kutendewa kazi?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka kuwa sanduku linamsitiri vizuri zaidi. Wakati mwingine inatokea maumbile ya mwanamke kuonekana kikamilifu katika harakati za mazishi. Ni jambo lisilopendekezwa. Haina shaka kuwa yale yanayofanywa Hijaaz, na khaswa Makkah, pindi wanapoliwekea jeneza kitu hiki kinamsitiri vizuri zaidi.

Kuhusu yale yenye kudhiri kwa mwanamke kama mfano wa nguo zake, sio haramu kuonekana sawa akiwa maiti au hai. Isipokuwa tu ikiwa ni nguo zinazofichua maumbile yake. Haifai kwake akavaa nguo kama hizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/173)
  • Imechapishwa: 07/08/2021