Ni ipi hukumu ya kunyanyua sauti wakati wa kusindikiza jeneza?

Swali: Baadhi ya watu wanabeba jeneza na kukimbia nalo. Kisha anakuwepo mmoja anayewaamrisha watu wote kusema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na wamtaje Allaah, ambapo wanafanya hivo. Je, hili lina asli?

Jibu: Kitendo hichi hakina asli na ni Bid´ah. Anayesindikiza jeneza anatakiwa kufikiria mwisho wake na kwamba ipo siku na yeye atabebwa kama anavyobebwa maiti huyu. Anatakiwa kufikiria dunia hii na namna mtu huyu jana alivyokuwa ardhini, na leo matendo yake ndio yatahesabiwa. Haya ndiyo yaliyowekwa katika Shari´ah. Haikupokelewa kutoka kwa Salaf wakati wa kusindikiza jeneza walisema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” au kuwashaji´isha wengine kumdhukuru Allaah. Kitendo bora anachoweza mtu kufanya ni yale yaliyofanywa na Salaf (Rahimahumu Allaah).

Kuhusu kuliharakisha jeneza, ni Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Lifanyisheni haraka jeneza.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/171-172)
  • Imechapishwa: 24/08/2021