Ni ipi hukumu ya kunyanyua sauti mazishini?

Swali: Watu wengi wananyanyua sauti wakati wa mazishi. Je, kuna ubaya?

Jibu. Hakuna neno kukiwa kuna haja. Mfano wa haja hiyo ni kama mtu kunyanyua sauti pindi anapoomba kokoto, ubumba au mawe. Hakuna neno midhali kuna haja. Vinginevyo bora ni kukaa kimya. Mambo ni namna hiyo ikiwa kunyanyua sauti sio juu ya kitu cha ´ibaadah, kama kuomba maji, kokoto au kitu kingine. Ama ikiwa wamenyanyua kwa lengo la ´ibaadah kama kusoma Qur-aan, au Dhikr basi kitendo hicho ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/172)
  • Imechapishwa: 24/08/2021