Ni ipi hukumu ya kutumia mashine ya kuchimba wakati wa kuchimba kaburi?

Swali: Ardhi ya makaburi ni yenye matope kupita kiasi na tayari imejaa. Hivi sasa hakukubakia kutumia kwa ajili ya makaburi isipokuwa ardhi ya mawe. Ni vigumu kuchimba kwa mikono katika ardhi kama hii. Je, inafaa kutumia compressor au mashine nyingine za kuchimba mfano wake?

Jibu: Ikiwa mnaweza kuchimba kwenye ardhi ya matope, basi yahamisheni makaburi kwenda huko. Kuchimba kwenye ardhi ya matope ni haraka zaidi katika kuchimba na kwepesi. Aidha mwanandani anahifadhika vyema zaidi kutokamana na mvua. Kwa hivyo ardhi ya matope ndio bora zaidi ijapo itakuwa masafa ya mbali. Na ikiwa hilo haliwezekani kwa sababu ardhi zenu zote ni za mawe, basi hapana neno kutumia mashine nzito. Hilo ni kutokana na dharurah ya jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/179)
  • Imechapishwa: 25/05/2022