Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ni Mwenye kusikia – hana shaka. Ni Mwenye kuona – hasiti. Ni mtambuzi – si Mwenye kutojua. Mwingi wa kutoa – hafanyi choyo. Ni mvumilivu – hafanyi haraka. Ni mwenye kuhifadhi – hasahau. Yuko macho – hapuuzilii mbali. Ni mwenye kuchunga – haghafiliki. Anazungumza, anatikisika, anasikia, anaona, anatazama, anakamata, anakunjua, anacheka, anafurahi, anapenda, anachukia, anabughudhi, anaridhia, anakasirika, anaghadhibika, anarehemu, anapuuza, anasamehe, anaghufuria, anatoa na anazuia.

Anashuka kila usiku katika mbingu ya chini, vile Anavotaka na kama alivotaka:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Nyoyo za waja ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma. Anavipindua Atakavyo, na Anawaruzuku kile Akitakacho.

Amemuumba Aadam kwa mkono Wake na kwa sura Yake.

Mbingu na ardhi siku ya Qiyaamah zitakuwa kwenye kiganja Chake na kwenye mkamato Wake.

Atauweka mguu Wake juu ya Moto wa Jahannam upungue.

Wako watu ambao Atawatoa nje ya Moto kwa mkono Wake.

Watu wa Peponi watautazama uso Wake. Watamtembelea. Atawaheshimisha, Atajionyesha kwao na awape zawadi.

Waja watahudhurishwa mbele Yake siku ya Qiyaamah. Yeye Mwenyewe ndiye atawafanyia hesabu. Hakuna mwingine atayefanya hivo zaidi ya Mola wetu (´Azza wa Jall). Yeye ni muweza kwa yale Ayatakayo.

[1] 42:11

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 59-64
  • Imechapishwa: 25/05/2022