Ni ipi hukumu ya kujenga juu ya makaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kujenga juu ya makaburi?

Jibu: Kujenga juu ya makaburi ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo kutokana na kule kuwatukuza wafu na sababu nyingine hiyo ni njia ya kuabudiwa makaburi haya na kufanywa ni washirika pamoja na Allaah. Hivo ndivo ilivyo hali ya majengo mengi yaliyojengewa juu makaburi. Hatimaye watu wakaanza kuwaomba wafu wale na kumshirikisha Allaah (Ta´ala). Kuwaomba wafu na kuwataka msaada ili kuondoa matatizo ni shirki kubwa na kuritadi nje ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/212)
  • Imechapishwa: 25/05/2022