Ni ipi hukumu ya kusoma Suurah “Yaa Siyn” na “alIkhlaasw” makaburini?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Suurah “Yaa Siyn” na “al-Ikhlaasw” makaburini? Kuna mtu amesema inatakiwa kusoma “al-Ikhlaasw” mara kumi na moja.

Jibu: Ni Bid´ah kusoma Qur-aan makaburini sawa iwe inahusiana na “Yaa Siyn”, “al-Ikhlaasw” au “al-Faatihah”. Haifai kusoma Qur-aan makaburini. Mtu atosheke na yale yaliyothibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

السَّلامُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الدِّيَارِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِين وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللهُ بكم لاحِقُونَ نَسْأَلُ الله لَنَا وَلَكُمْ الْعَافِية

“Amani ya Allaah iwe juu yenu manyumba ya wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana nanyi. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya.”[1]

اللهم لا تحرمنا أجره ولا تفتنـا بعـده و اغفر لنا و له

“Ee Allaah! Usitunyime ujira wake na wala usitujaribu baada yake. Utusamehe sisi na yeye.”[2]

Baada ya hapo mtu aende zake na asizidishe kitu juu ya haya. Si Qur-aan wala kitu kingine.

[1] Muslim (974).

[2] Ahmad (4/79), Abuu Daawuud (3201) na Ibn Maajah (1498)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/221-222)
  • Imechapishwa: 01/09/2021