Inajuzu kuwasomea “al-Faatihah” maiti?

Swali: Inajuzu kuwasomea “al-Faatihah” maiti? Inawafikia?

Jibu: Sijui dalili yoyote kutoka katika Sunnah juu ya kuwasomea maiti “alFaatihah”. Isisomwe. Asli katika ´ibaadah ni makatazo na kukomeka mpaka pale kutaposimama dalili juu ya kuthibiti kitendo fulani na kwamba ni katika Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall). Dalili ya hilo ni kuwa Allaah amewakemea wale wenye kutunga Shari´ah katika dini ya Allaah yale ambayo hakuyaidhinisha. Amesema (Ta´ala):

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Je, wanao washirika waliowatungia dini yale ambayo Allaah hakuyaidhinisha? Lau si neno la uamuzi, bila shaka kungelihukumiwa kati yao. Hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.”

Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa mwenyewe.”[1]

Ikishakuwa ni chenye kurudishwa kinakuwa ni batili na kisichokuwa na maana. Allaah (´Azza wa Jall) asiabudiwe kwa kitendo kama hicho.

Ama kumkodi mtu asije kumsomea Qur-aan yule maiti na thawabu zimwendee, ni jambo la haramu. Si sahihi kuchukua malipo juu ya kusoma Qur-aan. Mwenye kuchukua malipo juu ya kusoma Qur-aan ni mwenye kupata dhambi na wala hapati thawabu. Kusoma Qur-aan ni ´ibaadah na ´ibaadah haifai kuwa ni njia inayopelekea katika maslahi ya kidunia. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ

“Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa chochote humo.”[2]

[1] Muslim (1718).

[2] 11:15

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/219-220)
  • Imechapishwa: 01/09/2021