Ni ipi hukumu ya kuandika jina la maiti na tarehe ya kufa kwake juu ya jiwe la kaburi?

Swali: Tunaona namna ambavo baadhi ya watu wanaweka upande mmoja wa kaburi la maiti alama ya simenti ambayo wanaandika juu yake jina la maiti na tarehe ya kufariki kwake na wakati mwingine wanaweza kunyanyua jengo lake.

Jibu: Haya yamekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuandika juu ya kaburi[1]. Baadhi ya wanazuoni wameruhusu kuweka alama au jina peke yake.

Kuhusu kuandika tarehe ya kufariki kwake, jina la baba yake, jina la babu na mfano wake au kukaandikwa baadhi ya Aayah za Qur-aan ni miongoni mwa Bid´ah ambazo zinatakiwa kuondoshwa na kubadilishwe jiwe kwa jingine. Aidha jiwe linalowekwa halitakiwi kunyanyuliwa ziadi kuliko makaburi mengine. Jiwe hilo linatakiwa liwe sawa na mawe mengine. Kwa sababu ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia Abul-Hayyaaj al-Asadiy:

“Hivi nisikutume juu ya kazi aliyonituma kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (1052) ambaye amesema kuwa ni nzuri na Swahiyh.

[2] Muslim (969).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/190-191)
  • Imechapishwa: 24/05/2022