Wasalimishe wale wanaoswali kuelekea Qiblah. Usimkufurishe yeyote kwa dhambi. Usimtoe yeyote nje ya Uislamu kutokana na kitendo. Isipokuwa kukiwa kuna Hadiyth inayosema hivo. Katika hali hiyo Hadiyth hiyo itasimuliwa kama ilivyokuja; tutaisadikisha na kuikubali na kutambua kwamba ni kama ilivyokuja. Mfano wa Hadiyth hizo ni kama zinazozungumzia kuacha swalah na kunywa pombe. Mfano mwingine ni Bid´ah yenye kutumia mwenye nayo ndani ya ukafiri au ikamtoa nje ya Uislamu. Lazimiana na mapokezi katika jambo hilo na wala usizivuke.

Sipendelei kuswali nyuma ya Ahl-ul-Bid´ah wala kumswalia anayekufa miongoni mwao.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 24/05/2022