05. Msikilize na mtii kiongozi wako

Muda wa kuwa wapo watu wawili ulimwengu, basi ukhaliyfah ni kwa Quraysh. Haifai kwa mtu yeyote kuvutana nao juu ya hilo. Haifai kwa yeyote kufanya uasi dhidi yao. Hakuna ukhaliyfah wa mwingine utaokubaliwa mpaka kusimama kwa Saa.

Jihaad ni yenye kuendelea na viongozi, ni mamoja ni wema au waovu. Haubatilishwi kwa dhuluma ya mwenye kudhulumu wala uadilifu wa mwenye kufanya uadilifu.

Ijumaa na swalah za ´iyd mbili na hajj inasimamiwa na watawala hata kama hawatakuwa wema, waadilifu na wenye kumcha Allaah.

Kodi, swadaqah, sehemu moja ya kumi, fai na ngawira wanapewa viongozi, ni mamoja waadilifu au wakandamizaji.

Inatakiwa kumnyenyekea yule ambaye Allaah amempa utawala. Usimuasi. Usimfanyie uasi kwa upanga wako. Badala yake unatakiwa kusubiri faraja na njia ya kutokea kutoka kwa Allaah. Usimfanyie uasi mtawala. Sikiliza na utii. Usivunje kiapo alichopewa. Yule mwenye kufanya hivo ni mzushi na mwenye kufarikisha Mkusanyiko.

Mtawala akikuamrisha jambo ambalo ni kumuasi Allaah, haifai kwako kumtii kabisa. Lakini haina maana kuwa utamfanyia uasi na kumzuilia haki yake.

Kujizuilia kipindi cha fitina ni Sunnah yenye kuendelea ambayo inapaswa kulazimiana nayo. Ukijaribiwa basi itangulize nafsi yako na mali yako pasi na dini yako. Usishiriki kwa mikono yako katika fitina, wala kwa mkono wako na wala kwa mdomo wako. Lakini uzuie mkono wako, ulimi wako na matamanio yako – Allaah ndiye Mwenye kusaidia.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 45-48
  • Imechapishwa: 24/05/2022