Ni haramu kuunganisha swalah kwa swalah nyingine?

Swali: Ni haramu kuunganisha swalah kwa swalah nyingine?

Jibu: Hapana, haijuzu. Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo[1]. Haifai punde tu baada ya kumaliza swalah akasimama kuswali swalah nyingine pasi na kumuomba Allaah msamaha, kumtaja Allaah wala kuzungumza chochote.

Swali: Akisimama kutoka msikitini kabla ya kuleta Adhkaar anaweza kurejea kwa mara nyingine kuleta Adhkaar?

Jibu: Hapana vibaya. Yote ni mambo yaliyopendekezwa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kubadilisha-maeneo-baada-ya-swalah-ya-faradhi/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22575/ما-حكم-وصل-الصلاة-بالصلاة
  • Imechapishwa: 05/07/2023