Mgonjwa asiyeweza kutia maji puani wakati wa kutawadha

Swali: Ndugu yangu mmoja amepatwa na puani na anapata uzito kuingiza maji puani wakati wa kutawadha. Je, inatosha kwake  kulowesha vidole vyake kwa maji na akaviingiza puani?

Jibu: Ikiwa kunamuumiza basi afanye Tayammum na wala asijitie kwenye khatari ya maji ikiwa kufanya hivo kunamdhuru.

Swali: Anaweza kuingiza vidole vyake puani peke yake?

Jibu: Hapana, kupangusa peke yake haitoshi. Ni lazima apandishe maji puani. Lakini ikiwa hawezi basi afanye Tayammum. Akimaliza kutawadha basi afanye Tayammum kwa kunuia pua muda wa kuwa maji yanamdhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22576/كيف-يستنشق-المصاب-بحساسية-في-انفه
  • Imechapishwa: 05/07/2023