Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أنس رضي الله عنه عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (يَتْبَعُ المَيتَ ثَلاَثَةٌ: أهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَملُهُ، فَيَرجِعُ اثنَانِ وَيَبْقَى وَاحِدٌ: يَرجِعُ أهْلُهُ وَمَالُهُ، وَيَبقَى عَملُهُ). مُتَّفَقٌ عَلَيه

104 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maiti hushindikizwa na vitu vitatu; watu wake, mali yake na matendo yake. Viwivili vinarudi na kunabaki kimoja; watu wake na mali yake inarudi na kunabaki matendo yake.”

al-Bukhaariy na Muslim

Mtu anapokufa anafuatwa na wenye kumzika. Familia yako wanakufuata na kwenda kukuzika kwenye makaburi. Ni maajabu yaliyoje ya maisha ya duniani! Yana dharau na yako duni namna gani! Wanaosimamia mazishi yako ni wale watu ambao ni wapenzi zaidi kwako. Wanakupeleka na kwenda kukuzika. Wanakuweka mbali na wao. Lau hata wangelipewa pesa ili wabaki na wewe wasingeridhia hilo. Watu walio karibu zaidi kwako na ambao wewe ni mpenzi zaidi kwao ndio ambao wanasimamia mazishi yako na kuomboleza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/98)
  • Imechapishwa: 18/12/2023