03. Hadiyth “Swalah ya mwanamke katika pembe yake ni bora kuliko… “

342 – Ameeleza (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

صلاةُ المرأةِ في بيتها خيرٌ من صلاتِها في حجرتها، وصلاتُها في حُجرتها خيرٌ من صلاتِها في دارها، وصلاتُها في دارِها خير من صلاتِها في مسجد قَومها

“Swalah ya mwanamke katika pembe yake ni bora kuliko swalah yake katika chumba chake, na swalah yake katika chumba chake ni bora kuliko swalah yake katika nyumba yake, na swalah yake katika nyumba yake ni bora kuliko swalah yake katika msikiti ulio karibu naye.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awasatw” kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/259)
  • Imechapishwa: 18/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy