Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أنس رضي الله عنه عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (يَتْبَعُ المَيتَ ثَلاَثَةٌ: أهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَملُهُ، فَيَرجِعُ اثنَانِ وَيَبْقَى وَاحِدٌ: يَرجِعُ أهْلُهُ وَمَالُهُ، وَيَبقَى عَملُهُ). مُتَّفَقٌ عَلَيه

104 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maiti hushindikizwa na vitu vitatu; watu wake, mali yake na matendo yake. Viwivili vinarudi na kunabaki kimoja; watu wake na mali yake inarudi na kunabaki matendo yake.”

al-Bukhaariy na Muslim

Katika Hadiyth hii kuna dalili juu ya kwamba dunia itatoweka. Mazuri yote ya dunia hurudi na hakuna kitachobaki na wewe kwenye kaburi lako. Mali na watoto ni mapambo ya maisha ya dunia. Hivi vinarudi. Kinachobaki ni matendo.

Hivyo basi ni juu yako, ee ndugu yangu, kupupia kuangalia juu ya rafiki huyu atayebaki na harudi na wenye kurudi. Jitahidi mpaka uhakikishe hufanyi isipokuwa tu matendo mema yatayokusaidia ndani ya kaburi lako pindi utapokuwa mwenyewe mbali na wapenzi wako na familia yako na watoto wako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/98-99)
  • Imechapishwa: 18/12/2023