Swali: Je, ni sahihi kauli: “Jins-ul-´Amal” ni tamko la Bi´dah halikuwepo kwa Salaf; na ni tamko la utata yenye maana nyingi na ni bora kuiacha?

Jibu: Hatujui neno hili katika maneno ya wanazuoni wetu na wanazuoni wa Salaf. Sijui tofauti ya Jins-ul-´Amal na kitendo. Inasemwa “Kitendo” na si “Jins-us-´Amal”. Kunasemwa “Kitendo.” Kitendo ni katika imani. Imani ni kauli kwa ulimi na Itikadi katika moyo na vitendo vya mwili, na hawakusema “Jins-ul-´Amal.” Tamko hili halina msingi na huenda imetoka kwa Murji-ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majid%2021-03-1438H.mp3%2033.mp3.
  • Imechapishwa: 03/04/2022