45. Masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah ndio bora zaidi au masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan?

Swali: Masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah ndio bora zaidi au masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan?

Jibu: Yote mawili yana fadhilah zake. Baadhi ya wanazuoni wanaoanisha kwa kusema siku kumi za mwisho za Ramadhaan nyusiku zake ni bora zaidi. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikesha siku kumi za mwisho za Ramadhaan kwa kufanya ´ibaadah. Aidha usiku wa Qadar unatarajiwa katika siku kumi za mwisho za Ramadhaan, ijapo matarajio zaidi yapo katika zile nyusiku za witiri kuliko nyusiku za shufwa. Kwa ajili hiyo siku kumi za mwisho za Ramadhaan zikazingatiwa kuwa bora zaidi.

Kuhusu siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah, amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.” Wakamuuliza: “Hata kupigana Jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema: “Hata kupigana Jihaad katika njia ya Allaah. Isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake na asirudi na chochote katika hayo.”[1]

Amefanya umaalum katika ile michana yake. Pamoja na kwamba nyusiku kumi za mwisho za Ramadhaan zina ubora wake, lakini neno siku husemwa kwa kuachiwa na kukakusudiwa mchana.

[1] al-Bukhaariy (969).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 04/04/2022