Swali: Allaah (Subhaanah) amesema:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

”Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[1]

Je, hapa kuna dalili ya kumuozesha msichana mdogo?

Jibu: Ndio. Inafaa kwa baba kumuozesha msichana wake mdogo. Kama ambavo Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alimuozesha ´Aaishah kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na miaka sita. Alimuoa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na miaka sita na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjamii akiwa na miaka tisa. Inafaa kwa baba tu kumuozesha msichana ambaye hado hajafikisha umri wa kuyapambanua mambo.

[1] 65:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 27/05/2023