Kumrejea mke punde tu kabla ya kuzaa

Swali: Mwanamme akimtaliki mke wake hali ya kuwa ni mjamzito talaka moja na punde tu kabla ya kujifungua mtoto akamrejea. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Ndio, inafaa kwake kufanya hivo. Muda wa kuwa ni mwenye mimba na hajajifungua, yuko ndani ya eda.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 27/05/2023