Ndio maana bima ya afya ikawa ni haramu

Swali: Ni ipi hukumu ya bima ya afya?

Jibu: Bima ya afya haijuzu. Bima ya afya ni katika kamari. Kwa sababu wanatoa kiwango cha pesa maalum ili watibiwe kwa kila kinachowapata.

Swali: Mwenye nayo anasema kuwa wakati wa kipimo analipa asilimia ishirini tu na hivi sasa mke wake anakaribia kujifungua. Ajifungue kwa bima hiyo au hapana?

Jibu: Ajifungue hospitali nyenginezo.

Swali: Kwa hiyo ni haramu moja kwa moja?

Jibu: Ndio, inafanana na kamari.

Swali: Ni vipi bima ya afya inafanana na kamari?

Jibu: Kwa sababu mtu unalipia kiwango cha pesa kadhaa kila mwaka au kila mwezi kwa ajili ya kutibu kila kitu kinachomtokea mtu au familia. Matokeo yake anaweza kupatwa na magonjwa mengi yanayohitaji makumi ya maelfu.

Swali: Kila mmoja analipa 100.000. Hiyo ndio kamari? Hatulipi kitu kutoka katika mishahara yetu. Ni vipi inakuwa kamari?

Jibu: Inakuwa kamari na ile hospitali wanayoilipa pesa hizi. Wanapokwambia kila mwezi au kila mwaka watachukua 100.000 ili kuwatibu familia yote yale maradhi yanayowapata. Wanaweza kupatwa na maradhi mengi yanayohitaji pesa zaidi kuliko hizo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23280/ما-حكم-التامين-الصحي
  • Imechapishwa: 19/12/2023