Ibn Baaz kuhusu kumsomea Yaa Siyn anayetaka kukata roho

Swali: Kumsomea Suurah Yaa Siyn ambaye anataka kukata roho?

Jibu: Hapana neno – Allaah akitaka. Ni Hadiyth ambayo wako kikosi cha wanazuoni walioidhoofisha na wengine wakaisahihisha. Akimsomea anayetaka kukata roho Suurah Yaa Siyn hapana neno – Allaah akitaka.

Swali: Wakati wa kusoma “Buluugh-ul-Maram” kana kwamba umeidhoofisha Hadiyth hiyo?

Jibu: Kuna udhaifu katika Hadiyth hiyo. Katika cheni yake kuna Abu ´Uthmaan ambaye kuna maoni tofauti juu yake. Hata hivyo jambo ni jepesi kwa atakayeisoma kwa kujengea maoni ya ambao wameisahihisha Hadiyth hii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23278/حكم-قراءة-سورة-يس-على-المحتضر
  • Imechapishwa: 19/12/2023