Nasaha kwa vijana wenye kujishughulisha na aibu za watu

Swali: Una nasaha yoyote kuwapa vijana ambao wanapoteza wakati wao katika maneno ya kipuuzi, kutahadharisha wengine, kuwatukana watu na kuwatupia tuhuma mbalibali?

Jibu: Hili halijuzu. Huku ni kusengenya:

وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ

“Na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo!” (49:12)

Je, watu hawa wao hawana madhambi? Ni kwa nini wasizihesabu nafsi zao na wakaangalia mapungufu na madhambi yao na wakaacha kujishughulisha na watu?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020