Namna ya kumlipa wema kafiri aliyekufanyia wema

Swali: Ikiwa mtenda wema ni mtu mwema anatakiwa kulipwa wema?

Jibu: Haijalishi kitu akiwa kafiri. Mwombee uongofu, ikiwa amekupa pesa mrudishie nawe pesa kama alivyokupa, ikiwa amekuongoza njia au amekuelekeza katika jambo linalokunufaisha mwombee kwa Allaah amjaze kheri na amwongoze.

Swali: Allaah amwongoze?

Jibu: Allaah amwongoze, nakuombea kwa Allaah akuongoze, Allaah akujaze kheri; kuna kheri na mema ya duniani na mema ya Aakhirah.

Swali: Kwa hivyo mtu alipize wema…

Jibu: Ikiwa ni wema wa pesa amlipe kwa pesa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikubali zawadi na akilipa kutokana na zawadi hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23157/هل-يكافا-فاعل-المعروف-اذا-كان-كافرا
  • Imechapishwa: 17/11/2023