Swali: Kuna mtu ambaye siku zote anajiombea du´aa dhidi yake na watoto wake wanachelea asije kuitikiwa du´aa yake.

Jibu: Wamnasihi na wamwombee kwa Allaah asimchukulie, Allaah asimwitikie kwa mambo ambayo yanaweza kuwadhuru, Allaah amuhifadhi kwa kila ovu, Allaah ayafanye imara maombi yake na kwamba aufanye imara ulimi wake. Wamwombee du´aa na pia wamnasihi. Nasaha zinatakiwa kukubaliwa hata kutoka kwa mtoto na kutoka kwa mtu wa mbali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23158/حكم-رجل-يدعو-على-نفسه-داىما
  • Imechapishwa: 17/11/2023