25. Hadiyth “Kitu cha kwanza ambacho mja atafanyiwa hesabu kwacho siku ya Qiyaamah ni swalah… “

377 – Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

أوّل ما يحاسبُ به العبدُ يومَ القيامةِ الصلاةُ، يُنظَرُ في صلاتِه؛ فإنْ صَلَحَتْ فقد أفلحَ، وإنْ فسدتْ خابَ وخَسِرَ

“Kitu cha kwanza ambacho mja atafanyiwa hesabu kwacho siku ya Qiyaamah ni swalah. Swalah yake itapelelezwa. Ikiwa vizuri, basi amefaulu, na ikiwa vibaya, basi amekula matupu na kukhasirika.”[1]

Imepokelewa pia katika “al-Mu´jam al-Awsatw”[2].

[1] Swahiyh kupitia zingine.

[2] Inatiwa nguvu na Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyoipokea an-Nasaa´iy na wengineo. Ni nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/274)
  • Imechapishwa: 16/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy