Du´aa iliyozoeleka isiyokuwa na msingi

Swali: Du´aa inayosema:

للهم إني لا أسألك رد القضاء، ولكن أسألك اللُّطْف فيه

“Ee Allaah! Hakika mimi sikuombi kurudisha nyuma makadirio, lakini nakuomba kunifanyia upole kwayo.”

Jibu: Hii haina msingi. Aombe kama kwa kusema:

اللهم إني أسألك الخير كله، وأعوذ بك من الشر كله

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kutokana na kheri zote na najilinda Kwako kutokana na shari zote.”

Amwombe Mola wake mema na ajilinda Kwake kutokana na shari. Hili ndilo limewekwa katika Shari´ah.

Swali: Ni haramu kuomba hivo?

Jibu: Haina msingi. Aombe kama kwa kusema:

اللهم إني أسألك الخير كله، وأعوذ بك من الشر كله

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kutokana na kheri zote na najilinda Kwako kutokana na shari zote.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23163/حكم-قول-لا-اسالك-رد-القضاء-ولكن-اللطف
  • Imechapishwa: 17/11/2023