Kunyanyua mikono katika Qunuut wakati wa majanga

Swali: Kuomba du´aa wakati wa majanga?

Jibu: Ni sawa akaomba. Hapana vibaya.

Swali: Je, kumepokelewa andiko kuhusu kunyanyua mikono katika du´aa ya Qunuut?

Jibu: Ndio, imepokelewa kwamba alinyanyua mikono yake katika Qunuut dhidi ya majanga. Vivyo hivyo kuhusu Qunuut ya Witr. Msingi ni kama vivyo hivyo, kwa sababu zote ni Qunuut na zote ni du´aa. Andiko la wazi ni kuhusu Qunuut ya majanga na Qunuut ya Witr inakuwa vivyo hivyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23165/حكم-الدعاء-بقنوت-النوازل-ورفع-اليدين
  • Imechapishwa: 17/11/2023