Namna hii ndivo zilikuwa du´aa za Mtume

Swali: Je, ilikuwa ni katika uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) kurefusha katika du´aa? Baadhi ya maimamu wanarefusha katika du´aa kwa kutumia hoja:

“… kisha achague katika du´aa anayotaka.”

Jibu: Iwe kama alivosema ´Aaishah ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) alikuwa anapenda du´aa zilizokusanya na anaomba kwa yasiyokuwa hayo. Aombe du´aa zilizokusanya katika Qunuut na swalah ya kuomba mvua bila ya kuwatia watu uzito.

Swali: Bora ni kuomba katika Sujuud?

Jibu: Aombe katika Sujuud. Miongoni mwa sababu za kuitikiwa ni kuomba kwenye Sujuud na mwishoni mwa swalah kabla ya kutoa salamu. Maeneo yote haya ni miongoni mwa nyakati za kuitikiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23124/هل-من-هدي-النبي-ﷺ-التطويل-في-الدعاء
  • Imechapishwa: 07/11/2023