Swali: Mtu anaswali pamoja na manaswara au akaingia kanisani kwa ajili ya kujikombakomba kwao.

Jibu: Anaswali pamoja na manaswara?

Swali: Anaswali pamoja nao.

Jibu: Asiswali nao, asiwapake mafuta na wala asiingie kanisani pasi po haja kama vile kuwalingania kwa Allaah, kuwaelekeza au dharurah kama vile baridi kali, mvua inanyesha na kadhalika:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kufanya hivo?

Jibu: Afunzwe ya kwamba haijuzu. Kama alikusudia kuwafunza na kuwaelekeza iwe kwa mambo mengine. Awafunze bila ya yeye kuswali nao. Anayeswali kwa ajili ya ´Iysaa anakufuru. Kama ameswali kwa ajili ya Allaah ni uzushi na makosa.

Swali: Ikiwa ni mtu mwenye elimu si ni fursa ya kuwasimamishia hoja?

Jibu: Awafunze tu. Awafunze. Huu ni ujinga wake. Elimu yake itakuwa pungufu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kujifananisha na makafiri na akasema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Kama anataka kuwalingania basi afanye hivo pasi na kujifananisha, pasi na kuswali nao na pasi na ya kuhudhuria mikusanyiko yao ya sikukuu na mingine. Asihudhurie mikutano yao, asiswali pamoja nao na wala asishirikiane nao katika chochote ambacho ni katika nembo zao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23118/حكم-دخول-الكنيسة-والصلاة-فيها-للمجاملة
  • Imechapishwa: 07/11/2023