122. Hivi ndivo wanavofunga waislamu siku ya ´Aashuuraa´

4 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofunga siku ya ´Aashuuraa´ na akawaamrisha Maswahabah zake kuifunga, wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hiyo ni siku inayotukuzwa na mayahudi na manaswara.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Utapofika mwaka ujao – Allaah akitaka – tutafunga siku ya tisa.”Haukufika mwaka ujao mpaka akafa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Muslim, al-Bayhaqiy na wengineo.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Siku ya ´Aashuuraa´ ni siku tukufu ambayo inafuta madhambi ya mwaka uliotangulia. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) alifunga siku hiyo, akaamrisha kuifunga na akaipendekeza. Wakati alipoambiwa kuwa punde kidogo kabla ya kuaga kwake dunia ya kwamba ni siku ambayo inaadhimishwa na mayahudi na manaswara, ndipo akaamrisha kujitofautisha nao kwa njia ya kufunga siku nyingine ziada. Akaazimia jambo hilo. Kwa ajili hiyo wanazuoni, akiwemo Imaam Ahmad, wameona kuwa inapendeza mtu afunge tarehe tisa na tarehe kumi. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walitoa sababu hiyo pia. Sa´iyd bin Mansuur amesimulia kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Fungeni tarehe tisa na tarehe kumi na jitofautisheni na mayahudi.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 41)

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. al-Bayhaqiy pia ameipokea. Imepokelewa mfano wake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa cheni ya wapokezi dhaifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 177-178
  • Imechapishwa: 07/11/2023