3 – Laylaa, mke wa Bashiyr bin al-Khaswaaswiyyah (Radhiya Allaahu ´anhum), amesema:

”Nilitaka kufunga siku mbili kwa kuunganisha ambapo Bashiyr akanikataza na kusema: ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinikataza jambo hilo na akasema: ”Manaswara ndio wanaofanya hivo. Fungeni kama alivyokuamrisheni Allaah, kamilisheni swawm kama alivyokuamrisheni Allaah na kamilisheni swawm mpaka usiku. Utapofika usiku basi fungueni.”[1]

[1] Ahmad na Sa´iyd bin Mansuur kupitia kwa ´Ubaydullaah bin Iyaad, kutoka kwa baba yake. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Laylaa ni Swahabah wa kike, kama ilivyotajwa katika ”at-Taqriyb” na katika vitabu vingine. Haafidhw Ibn Hajar ameinasibisha Hadiyth hiyo kwa at-Twabaraaniy, ´Abd bin Humayd na Ibn Abiy Haatim kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwenda mpaka kwa Laylaa.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Ametoa sababu ya makatazo ya kuunganisha swawm kwamba ni swawm ya manaswara. Mambo ni kama alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pengine inatokana na utawa wao waliouzua.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 176-177
  • Imechapishwa: 07/11/2023