120. Waislamu wanaharakisha kukata swawm

2 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dini itaendelea kuwa yenye kushinda muda wa kuwa watu wanaharakisha kufungua. Kwa sababu mayahudi na manaswara huchelewesha.”[1]

[1] at-Tirmidhiy na Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri. Nimezungumzia njia zake na kuzipambanua katika ”at-Ta´liyqaat al-Jiyaad ´alaa Zaad-il-Ma´aad”.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hii ni dalili ya wazi ya kwamba kushinda kwa dini kutaendelea kupatikana kwa kuharakisha kufungua swawm kwa ajili ya kujitofautisha na mayahudi na manaswara. Ikiwa kujitofautisha nao ni sababu ya dini kuwa juu – na sababu ya Allaah kuwatuma Mitume ni ili dini Yake iweze kuzishinda nyenginezo zote – basi hiyo ina maana kwamba kule kujitofautisha nao kwa dhati yake ni miongoni mwa malengo makubwa ya Mitume.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 176
  • Imechapishwa: 07/11/2023