72. Ni Suurah gani kamili kutoka katika Qur-aan iliyoteremshwa kamili?

Swali 72: Ni Suurah gani kamili kutoka katika Qur-aan iliyoteremshwa kamili?

Jibu: ´Abdullaah bin ´Amr amesema:

”Cha mwisho kilichoteremshwa kutoka katika Qur-aan ni Suurah ”al-Maaidah” na ”al-Fath”.”[1]

Bi maana:

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ

”Itakapokuja nusura ya Allaah na ushindi.”[2]

Hayohayo ndio yamesemwa na ´Aaishah kuhusu ”al-Maaidah”.[3]

Hayohayo yamesemwa na Ibn ´Abbaas kuhusu:

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ

”Itakapokuja nusura ya Allaah na ushindi.”[4] [5]

al-Baraa´ bin ´Aazib amesema:

”Suurah ya mwisho iliyoteremshwa ilikuwa ni ”al-Baraa-ah”.”[6]

[1] at-Tirmidhiy (3063). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3063).

[2] 110:1

[3] al-Haakim (2/311).

[4] 110:1

[5] at-Tirmidhiy (3063). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3063).

[6] al-Bukhaariy (4654) na Muslim (1618).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 143
  • Imechapishwa: 07/11/2023