123. Ndio maana Mtume akifunga jumamosi na jumapili

5 – Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga siku ya jumamosi na jumapili zaidi kuliko anavyofunga masiku mengine. Amesema: ”Masiku hayo mawili ni sikukuu za washirikina. Mimi napenda kujitofautisha nao.”[1]

[1] Ahmad, al-Haakim na kupitia kwake al-Bayhaqiy kupitia kwa ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Umar bin ´Aliy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Kurayb, kutoka kwake [Umm Salamah]. Cheni hii ya wapokezi ni nzuri. al-Haakim amesema:

”Swahiyh.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye. Ibn Khuzaymah pia ameisahihisha, kama ilivyo katika ”Nayl-ul-Awtwaar” ambapo Hadiyth imenasibishwa kwa Ibn Hibbaan pia. Ibn-ul-Qayyim ameiegemeza katika ”as-Sunan” ya an-Nasaa’iy, na akafuatwa na Ibn Hajar katika ”Fath-ul-Baariy”. Udhahiri ni kuwa wanakusudia ”as-Sunan al-Kubraa” kwa sababu sijaipata katika ”as-Sunan as-Swughraa”. Kwa ajili hiyo an-Naabulsiy hakuitaja katika ”adh-Dhakhaair”, kwa sababu humo hutaja tu Hadiyth kutoka katika ”as-Sunan as-Swughraa”, kama alivyothibitisha katika utangulizi wake. al-Haythamiy ameitaja katika ”Majma´-uz-Zawaa’id” na akasema:

”Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr”. Wasimulizi wake ni wenye kuaminika. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan.

Huu ni upungufu wake kwa sababu hakuiegemeza katika ”al-Musnad”. Ni kana kwamba alipitwa na jambo hilo. Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Sikukuu mbili za washirikina kunakusudiwa jumamosi ni siku ya mahayudi na jumapili ni siku ya manaswara. Siku za ´iyd hazifungwi na hivyo akajitofautisha nao kwa kuzifunga siku mbili hizo. Haya yanajulisha kwamba yale maoni ya baadhi ya Shaafi´iyyah kwamba inachukiza kufunga jumamosi peke yake au jumapili peke yake si mazuri. Bora kuitumia hukumu hiyo kwa ambaye anafunga ijumaa peke yake, kama zilivyothibiti Hadiyth Swahiyh juu yake. Ama kuhusu jumamosi na jumapili bora ni kuzifunga, zote kwa pamoja na kwa kuzipwekesha, kwa ajili ya kutekeleza amri ya kujitofautisha na watu wa Kitabu… Nimezikusanya zile Hadiyth zinazoamrisha kujitafautisha na watu wa Kitabu na nikapata zaidi ya thelathini. Nimezitaja katika kitabu changu kinachoitwa ”al-Qawl ath-Thabt fiys-Swawmi Yawm-is-Sabt”.”  (Fath-ul-Baariy (10/298)

Nilichoweza kukusanya ni karibu hukumu thelathini nilizozitoa kutoka katika Hadiyth thelathini katika kitabu hiki – himdi zote njema anastahiki Allaah kwa tawfiyq na uongofu wake.

Kisha baadaye ikanidhihirikia kuwa kuna unyonge katika Hadiyth. Nimebainisha udhaifu wake katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (1099) na kwamba haikuwekwa katika Shari´ah kufunga siku ya jumamosi isipokuwa tu katika swawm ambayo ni ya faradhi, kama ambavo at-Twahaawiy amewanukuu baadhi ya wanazuoni katika ”Sharh-ul-Ma´aaniy”. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza makatazo yenye kuenea pale aliposema:

”Msifunge siku ya jumamosi isipokuwa katika yale mliyofaradhishiwa.”

Imetajwa katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl (960). Rejea maelezo yangu katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1/509).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 178-179
  • Imechapishwa: 08/11/2023