Namna hii ndivo utathibitisha mapenzi yako kwa Allaah

Ibn-ul-Waliyd amesema:

“Mashaykh walikuwa wakikerwa na maneno ya al-Hajjaaj na wakimkaripia kwa sababu alikuwa akichukua mambo yanayokwenda kinyume na Shari´ah na njia ya wenye kuipa kisogo dunia. Alikuwa akidai kumpenda Allaah, lakini akidhihirisha mambo yanayokwenda kinyume na madai yake.”

Hapana shaka yoyote kwamba kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio alama ya kumpenda Allaah, kwa sababu amesema (Ta´ala):

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 03:31-32

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/316)
  • Imechapishwa: 15/11/2020