“Nakuombeni kwa ajili ya Allaah”

Swali: Je, inafaa kuomba kwa uso wa Allaah?

Jibu: Haitakiwi kuomba kwa uso wa Allaah wala kuomba kwa ajili ya Allaah, isipokuwa tu wakati wa haja.

Swali: Vipi kuhusu kumjibu mtu huyo? Mtu akiomba kwa uso wa Allaah inatakiwa kumwitikia?

Jibu: Akiomba kwa uso wa Allaah apewe. Hilo ni kutokana na Hadiyth isemayo:

“Mwenye kuomba kwa uso wa Allaah mpeni.”

Hapo ni pale ambapo kuna wepesi wa kufanya hivo. Hata hivyo mtu huyo anatakiwa kufunzwa kwamba mara nyingine haitakiwi kuomba kwa uso wa Allaah. Ashauriwe kwamba asiombe kwa uso wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23233/ما-حكم-السوال-بوجه-الله-تعالى
  • Imechapishwa: 03/12/2023