Afanye nini ambaye amesahau Sujuud ya mwisho ya swalah?

Swali: Imamu aliwaswalisha watu akaacha sijda ya mwisho kisha wakamkumbusha ambapo akaleta Takbiyr na kuleta sijda tatu na kutoa salamu. Je, kitendo hichi ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Hapana. Asujudu sijda aliyoacha kisha atoe salamu halafu asujudu Sujuud mbili za kusahau.

Swali: Haimlazimu kuswali Rak´ah nyingine?

Jibu: Haimlazimu. Maoni sahihi ni kwamba haimlazimu. Asujudu sijda aliyoacha, atoe salamu kisha asujudu sijda mbili. Hivi ndio bora. Ni sahihi pia endapo atasujudu sijda ya kusahau, kisha akasujudu sujuud aliyoacha, kisha akasujudu sijda ya kusahau, kisha akatoa salamu. Kwa sababu kuchelewesha sujuud ya kusahau ni kwa njia ya ubora peke yake.

Swali: Hivi sasa amesujudu sijda tatu kwa pamoja kisha akatoa salamu…

Jibu: Hapana vibaya. Ni lazima alete Tashahhud baada ya sijda aliyoacha. Atasoma Tashahhud kisha atasujudu sijda ya kusahau kabla au baada ya salamu, ingawa akiileta baada yake ndio bora.

Swali: Hakufanya kama ulivosema.

Jibu: Basi anatakiwa kuirudia swalah yake kama kumeshapita muda mrefu. Na kama hakujapita kitambo kirefu ataleta Tashahhud, kisha akatoe salamu kisha asujudu sijda mbili za kusahau.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23232/ما-يفعل-من-نسي-السجدة-الاخيرة-بالصلاة
  • Imechapishwa: 03/12/2023