Najisi inapoingia ndani ya maziwa na vitu vya majimaji

Swali: Maziwa na venginevyo katika vitu vya majimaji vina hukumu moja kama maji vinapoingiwa na najisi?

Jibu: Maziwa na venginevyo katika vitu vya majimaji pindi najisi inapoingia ndani yake basi vina hukumu moja kama ya maji. Hiyo ina maana kwamba vinanajisika ikiwa ile rangi yake, ladha yake na harufu yake itabadilika kwa najisi hiyo. Vivyo hivyo ikiwa kiwango chake ni kidogo vinanajisika wakati najisi inapoingia ndani yake. Ikiwa havitobadilika harufu, ladha na rangi yake basi itakuwa ni haramu kuvinywa na kuvitumia.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (22/128) nr. (20049)
  • Imechapishwa: 01/06/2022