Swali: Je, nadhiri zote ni zenye kusemwa vibaya?

Jibu: Zote ni zenye kusimangwa, huo ndio udhahiri wa Hadiyth. Haitakikani kuweka nadhiri. Lakini akiweka nadhiri  na muda huohuo ni utiifu imeshafungika. Katika hali hiyo anapaswa kuitekeleza. Na ikiwa sio utiifu haitakiwi kuitekeleza. Badala yake anapaswa kutoa kafara ya kiapo. Nadhiri inaingia ndani ya zile hukumu tano:

1 – Uharamu.

2 – Ulazima.

3 – Machukizo.

4 – Mapendezo.

5 – Yenye kuruhusu.

Akisema kwamba ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kufunga siku fulani au kutoa swadaqah kitu fulani. Hiyo ni nadhiri ya utiifu. Katika hali hiyo analazimika kuitekeleza.

Akisema kwamba ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kunywa pombe. Hii n nadhiri ya haramu. Katika hali hiyo asinywe pombe. Badala yake anatakiwa kutoa kafara ya kiapo.

Akisema kwamba ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah kumsusa mtu fulani au asimtembelee fulani. Hii ni nadhiri inayochukiza. Katika hali hiyo anapaswa kutoa kafara ya kiapo na asimkate nduguye.

Akisema kwamba ni lazima kwangu kwa ajili ya Allaah asile chakula cha mtu fulani. Katika hali hiyo anayo khiyari; akitaka atatekeleza nadhiri yake na akitaka atatoa kafara ya kiapo na baada ya hapo ale chakula hicho.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24398/هل-النذر-مذموم-كله
  • Imechapishwa: 14/10/2024