Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
100 – Kheri na shari ni mambo yamekadiriwa kwa viumbe.
101 – Uwezo ambao unapelekea kitendo, kutokana na uongofu ambao haifai kumsifu kwao kiumbe, unakuwa pamoja na kitendo. Lakini kuhusu uongofu kwa njia ya uzima, kuweza, ustadi na usalama, unakuwa kabla ya kitendo na umefungamana na uzungumzishwaji. Ni kama alivosema (Ta´ala):
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]
MAELEZO
Jambo la kwanza limetajwa na Ashaa´rah na jambo la pili limetajwa na Mu´tazilah na wengineo. Maoni ya sawa ni yote mawili, kama alivofafanua mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) hapa. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameyabainisha kwa uzuri kabisa, na kwa ajili hiyo naona kuwa haina neno iwapo nitayanukuu hapa. Amesema (Rahimahu Allaah):
”Maswahibah zetu na wengine wamezungumza juu ya uwezo wa mja; ni pamoja na kitendo au ni kabla yake? Wamefanya kuwepo maoni mawili yanayogongana.
Baadhi wanaona kuwa uwezo unakuwa pamoja na kitendo peke yake. Haya ni maoni mara nyingi ya wafuasi wa wanafalsafa wa Ashaa´irah, wanaothibitisha makadirio, kati ya maswahiba zetu na wengineo.
Wengine wamefanya uwezo unakuwa kabla ya kitendo. Haya ni maoni mara nyingi ya Mu´tazilah na Shiy´ah, wanaokanusha makadirio.
Kundi la kwanza wamefanya uwezo unaendana na kitendo kimoja pekee, kwa sababu vimeambatana na haviachani. Kundi la pili wamefanya uwezo unakuwa wenye kuendana na vinyume viwili na kwamba kamwe hauambatani na kitendo. Hakuna waliopinda zaidi kama Qadariyyah; wanapinga uwezo kuambatana na kitendo. Wanaona kuwa ni lazima kile chenye kuathiri kitangulie kabla ya athari – haviwezi kuambatana pamoja. Hilo si kwa uwezo peke yake, bali pia matakwa na amri. Maoni sahihi yanayofahamishwa na Qur-aan na Sunnah, ni kwamba uwezo unatangulia kabla ya kitendo na wakati wa kitendo. Aidha kuna uwezo mwingine ambao hauendani na kitendo kingine. Kwa sababu kuna uwezo aina mbili: uwezo wenye kutangulia ambao unasilihi kwa vinyume viwili, na mwingine wenye kuambatana na hauwi isipokuwa pamoja na kitendo. Hiyo ndio ambayo inasahihisha na kupelekea kwenye kitendo, na nyingine inawajibisha na kuhakikisha kitendo. Allaah (Ta´ala) amesema juu ya hiyo ya kwanza:
وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا
”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea.”[2]
Ingelikuwa uwezo huu hauwi isipokuwa pamoja na kitendo tu, basi hajj ingelimuwajibikia tu yule ambaye amekwishahiji. Kwa msemo mwingine asingetenda dhambi mtu kwa kuacha kuhiji. Wala hajj isingelikuwa wajibu kabla ya Ihraam bali kabla ya kuimaliza. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]
Ameamrisha kumcha kwa kiasi cha uwezo wa mtu. Ingelikuwa makusudio ni uwezo uliofungamana na kitendo, basi uchaji usingelimuwajibikia yeyote kabla ya kitendo, kwa sababu jambo hilo ndio linaenda sambamba na uwezo huo. Allaah (Ta´ala) amesema:

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[4]
Bi maana hicho ndicho ulichoweza. Ingelikuwa makusudio ni yale yaliyoambatana, basi asingewajibika yeyote isipokuwa tu kile kitendo kinachofanywa na mtu na si yale mambo ya wajibu aliyoacha… Kuna mifano mingi juu ya hilo. Hakuna amri yoyote ndani ya Qur-aan na Sunnah, ambayo imewajibishwa kipindi cha kuwa na uwezo na kutowajibishwa kipindi cha kutokuwa na uwezo, hakikusudia kuambatanisha, vinginevyo Allaah asingewajibisha mambo ya wajibu isipokuwa tu kwa yule aliyeyafanya. Hata hivyo asingepata dhambi yule mwenye kuyaacha.
Kuhusu uwezo ulioambatana na kuwajibishwa, ni mfano wa maneno Yake (Ta´ala):
مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ
”… hawakuwa wakiweza kusikia na hawakuwa wakiona haki.”[5]
الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَن ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا
”… ambao macho yao yalikuwa katika pazia wasiweze kunidhukuru na walikuwa hawawezi kusikia.”[6]
Huu ndio uwezo ulioambatanishwa na uliyowajibishwa, kwa sababu uwezo mwingine unahitaji ´ibaadah iwe ni yenye kumuwajibikia mtu.
Wa kwanza ni Shari´ah na umefungamana na amri na makatazo, thawabu na makatazo. Ndio ambao huzungumziwa na wanazuoni na kwenye ndimi za watu. Wa pili ni wa kilimwengu na umefungamana na mipango na makadirio. Yenyewe ndio kunapatikana matendo. Wa kwanza umefungamana na amri zilizowekwa katika Shari´ah na wa pili umefungamana na maumbile ya kilimwengu. Kama alivosema (Ta´ala):
وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ
”Akasadikisha maneno ya Mola wake na Vitabu Vyake.”[7]
Watu wamekinzana juu ya uwezo wa mja kama anaweza kuyafanya jambo ambalo linatofautiana na yale anayoyajua Allaah au kuyataka. Ukweli wa mambo ni kwamba mja anaweza kuwa na ule uwezo wa kwanza na uliowekwa katika Shari´ah ambao ni wenye kutangulia kabla ya kitendo. Allaah pia ni muweza wa kufanya kitu kinachotofautiana na yanayotambulika na yanayotakiwa, vinginevyo Asingekuwa muweza isipokuwa tu wa yale anayoyafanya. Mja hawezi kuyafanya yale matakwa yaliyoambatana na kitendo, kwa sababu hakuna yanayotokea isipokuwa tu yale ambayo ameyajua na ameyataka. Anayotaka kutokea, yanatokea, na yale asiyoyataka kutokea, hayatokei. Vivyo hivyo maneno ya wanafunzi na wafuasi:
هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ
”Je, anaweza Mola wako kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni?”[8]
Walikuwa wakiuliza juu ya uwezo kama huu. Vivyo hivyo kuhusu Yuunus (´alayhis-Salaam):
إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهَ
“Alipoondoka akiwa ameghadhibika akadhani kuwa hatutamdhikisha (لَّن نَّقْدِرَ).”[9]
Bi maana hatuwezi kumuadhibu. Ni kama ambavo mtu anamuuliza mwingine kama anaweza kufanya jambo fulani na akimuhoji kama kweli atakifanya. Ni jambo lililotangaa kwenye midomo ya watu.
Wakati Qadariyyah waliposema kuwa uwezo aina ya kwanza unatosha katika kukifanya kitendo na kwamba mja anaumba matakwa yake mwenyewe, wakaona kuwa ni mwenye kujitosheleza na Allaah wakati anapotenda. Na pindi Jabriyyah walipoona kuwa uwezo aina ya pili unatosheleza kupelekea katika kitendo, ambacho hakifanywi na yeye, ndipo wakaona kuwa ametenzwa juu ya kitendo chake. Yote mawili ni makosa mabaya. Hakika mja anayo utashi na ni wenye kufuatia baada ya utashi wa Allaah, kama alivotaja Allaah maeneo mengi ndani ya Kitabu Chake:
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ
”Basi anayetaka atawaidhika. Na hawatowaidhika isipokuwa akitaka Allaah.”[10]
إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
“Hakika huu ni ukumbusho, basi anayetaka achukue njia ya Mola wake. Na hamtoweza kutaka chochote isipokuwa atake Allaah – hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hekima.”[11]
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ لِمَن شَاء مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاؤُونَ إِلَّا أَن يَشَاء اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
“Haikuwa huu isipokuwa ni Ukumbusho kwa walimwengu wote – kwa yule miongoni mwenu anayetaka anyooke. Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[12]
Ikiwa Allaah amemfanya mja kuwa ni mwenye kutaka na kutamani, basi haiwezekani kusema kuwa ametenzwa na kunyanyaswa. Kadhalika haiwezekani ikawa yeye ndiye kajiumbia matakwa yake.
Endapo mtu atapinga kwa kusema kwamba ametenzwa nguvu kuchagua na amelazimishwa kutaka, basi kipingamizi hicho hakina maana yoyote. Wala makusudio ya kutenzwa nguvu sio hayo – na hakuna yeyote anayeweza hilo isipokuwa Allaah. Kwa ajili hiyo Qadariyyah na Jabriyyah wametofautiana vinyume viwili. Wote wawili wamepatia katika yale waliyoyathibitisha pasi na katika yale waliyoyakanusha. Upande mmoja Abul-Husayn al-Baswriy na wenzake katika Qadariyyah wanasema hapana shaka kwamba mja ndiye huzalisha matendo na tabia yake mwenyewe na kwamba ni elimu ya kisasa kupinga uhakika huo. Upande mwingine, Ibn Khatwiyb na wenzake katika Jabriyyah wanadai kuwa hapana shaka kuwa elimu yenye nguvu zaidi ya mja kutenda badala ya kuacha inahitajia mtu mwingine kumfanya azingatie utekelezaji huo. Kwa sababu mtu ambaye ana uwezo wa pande mbili zinazolingana upande mmoja hauwezi kuwa na nguvu juu ya upande mwingine isipokuwa kwa kitu chenye kutia nguvu. Nadharia zote mbili ni sahihi, lakini si sahihi kudai kuwa kimoja kinapinga kingine. Mja ni mwenye kutenda na mwenye kuchuma matendo yake, lakini uzalishaji wake unahitaji mzalishaji mwingine. Mja ni mtendaji, mtengenezaji na mzalishaji, lakini kusema kuwa anayafanya yote hayo baada ya kutokuwepo maana yake ni kwamba yeye mwenyewe anahitaji ambaye amemuumba. Kama alivosema (Ta´ala):
لِمَن شَاء مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ
”… kwa yule miongoni mwenu anayetaka anyooke.”
Akitaka kunyooka, ndipo anakuwa mwenye kunyooka:
وَمَا تَشَاؤُونَ إِلَّا أَن يَشَاء اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
”Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[13]
Yote yaliyofahamishwa na dalili za kiwahy na za kiakili ni ya haki. Kwa ajili hiyo hakuna matikiso wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Mja ni mwenye hitaji la kidhati juu ya dhati ya Allaah, sifa na matendo Yake, licha ya kwamba yeye mwenyewe anayo dhati, sifa na matendo. Kukanusha matendo ni kama kupinga sifa na dhati yake. Huko ni kupinga haki na kumefanana na upetukaji wa wale Suufiyyah waliochupa mipaka ambao wanamzingatia yeye ndiye wa Haki. Na kudai kuwa hamuhitajii Allaah au anaweza kuwepo pasi Naye vilevile ni kupinga haki na kumefanana na uchupaji mipaka wa ambaye alisema:
أنا ربكم الأعلى
“Mimi ndiye Mola wenu mkuu.”[14]
Pamoja na yule ambaye anasema kuwa amejiumba mwenyewe. Haki ni yale waliyomo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.”[15]
[1] 2:286
[2] 3:97
[3] 64:16
[4] 2:286
[5] 2:286
[6] 18:101
[7] 66:12
[8] 5:112
[9] 21:87
[10] 74:55-56
[11] 76:29-30
[12] 81:27-29
[13] 81:27-29
[14] 79:24
[15] Majmuu´-ul-Fataawaa (8/371-376).
- Mhusika: Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 88-95
- Imechapishwa: 16/10/2024

Mhusika: Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 88-95
Imechapishwa: 16/10/2024
https://firqatunnajia.com/63-uwezo-wa-mja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)