Swali: Ni nini maana ya maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ

“Hatukuijaalia ndoto ambayo tulikuonyesha isipokuwa ni [kutaka kuwatia] mtihani kwa watu.”[1]

Jibu: Inawahusu washirikina ambao wamekadhibisha na wakahoji ni vipi ameona kadhaa baada ya kusema kuwa ameona Pepo, Moto, kwamba amemuona Jibriyl katika umbile fulani katika safari ya kupandishwa mbinguni usiku. Vilevile alisimulia kuwa  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona Yerusalemu kadhaa na kadhaa. Watu wengi wakapinga na wakapewa mtihani kwa sababu hiyo:

لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ

“Hakika aliona miongoni mwa alama za Mola wake kubwa kabisa.”[2]

[1] 17:60

[2] 53:18

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24402/تفسير-وما-جعلنا-الرويا-التي-اريناك-الا-فتنة
  • Imechapishwa: 14/10/2024