Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

99 – Allaah (Ta´ala) ameumba Pepo na Moto kabla ya kuumba vitu vyengine. Aidha akaviumbia wakazi wake. Yule ambaye Anamtaka ataingia Peponi, atafanya hivo kutokana na fadhilah Zake, na yule ambaye Anamtaka ataingia Motoni, atafanya hivo kutokana na uadilifu Wake. Kila mmoja anatenda kwa yale ambayo amekwishakadiriwa na anapita juu ya yale aliyoumbiwa kwayo.

MAELEZO

Anaashiria maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Allaah amekwishamkadiria kila mja mambo matano: muda wake wa kueshi, riziki yake, mabaki yake, namna ya kufa kwake na kama atakuwa mla khasara au mwenye furaha.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh na imekaguliwa katika “al-Mishkaah” (113) na “as-Sunnah” (303-309). Zipo Hadiyth nyingi na zinazotambulika zenye maana kama hiyo.

[1] Ahmad (21723), Ibn Hibbaan (6150) na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (3120).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 14/10/2024