Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
97 – Tunaamini kufufuliwa, kulipwa kwa matendo, uonyeshwaji, hesabu, kusoma ndani ya madaftari, thawabu, adhabu na Njia na Mizani siku ya Qiyaamah.
98 – Pepo na Moto vimeshaumbwa. Kamwe havitoteketea wala kumalizika.
MAELEZO
Tambua kuwa kuna Moto aina mbili. Moto ambao utateketea, na Moto mwingine ambao utabaki milele. Moto aina ya kwanza ni wa waislamu watenda madhambi, na Moto aina ya pili ni wa makafiri na washirikina. Huu ni ufupisho wa aliyoyahariri katika ”al-Waabil as-Swayyib” cha Ibn-ul-Qayyim. Maoni haya ndio haki ambayo hakuna shaka yoyote juu yake na dalili zimekusanyika juu yake. Kwa ajili hiyo usidangnyike na yale aliyotaja Ibn Abiyl-´Izz hapa na Ibn-ul-Qayyim katika ”Shifaa’-ul-´Aliyl” na ”Haadiyl-Arwaah”, ambayo yanaweza kupingana na haya ambayo nimeyafupisha hapa. Mosi hawana maoni hayo, pili ni kwamba hakuna dalili ya wazi na sahihi inayosema kuwa Moto wa makafiri utateketea. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wakazi wa Peponi:
وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
“… nao humo hawatotolewa.”[1]
amesema hayohayo juu ya makafiri:
وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ
“… na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.”[2]
Yale yaliyopokelewa kutoka kwa ´Umar na wengineo hazikusihi cheni zake za wapokezi, kama nilivyobainisha katika taaliki yangu ya ”Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” na ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah”[3].
[1] 15:48
[2] 2:167
[3] Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah (606-607).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 86-87
- Imechapishwa: 14/10/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
97 – Tunaamini kufufuliwa, kulipwa kwa matendo, uonyeshwaji, hesabu, kusoma ndani ya madaftari, thawabu, adhabu na Njia na Mizani siku ya Qiyaamah.
98 – Pepo na Moto vimeshaumbwa. Kamwe havitoteketea wala kumalizika.
MAELEZO
Tambua kuwa kuna Moto aina mbili. Moto ambao utateketea, na Moto mwingine ambao utabaki milele. Moto aina ya kwanza ni wa waislamu watenda madhambi, na Moto aina ya pili ni wa makafiri na washirikina. Huu ni ufupisho wa aliyoyahariri katika ”al-Waabil as-Swayyib” cha Ibn-ul-Qayyim. Maoni haya ndio haki ambayo hakuna shaka yoyote juu yake na dalili zimekusanyika juu yake. Kwa ajili hiyo usidangnyike na yale aliyotaja Ibn Abiyl-´Izz hapa na Ibn-ul-Qayyim katika ”Shifaa’-ul-´Aliyl” na ”Haadiyl-Arwaah”, ambayo yanaweza kupingana na haya ambayo nimeyafupisha hapa. Mosi hawana maoni hayo, pili ni kwamba hakuna dalili ya wazi na sahihi inayosema kuwa Moto wa makafiri utateketea. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wakazi wa Peponi:
وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
“… nao humo hawatotolewa.”[1]
amesema hayohayo juu ya makafiri:
وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ
“… na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.”[2]
Yale yaliyopokelewa kutoka kwa ´Umar na wengineo hazikusihi cheni zake za wapokezi, kama nilivyobainisha katika taaliki yangu ya ”Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” na ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah”[3].
[1] 15:48
[2] 2:167
[3] Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah (606-607).
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 86-87
Imechapishwa: 14/10/2024
https://firqatunnajia.com/61-maoni-ya-sawa-ya-ibn-ul-qayyim-juu-ya-moto/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)