Swali 654: Je, nadhiri ya huduma ni maalum kwa nyumati zilizotangulia?

إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Wakati aliposema mke wa ´Imraan: ”Mola wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kile kilichomo ndani ya tumbo langu kuwa ni waqf kukutumikia, hivyo basi Nitakabalie. Hakika Wewe ni Msikivu wa yote, Mjuzi wa yote.”[1]

Jibu: Hapana. Iwapo mwanamume atamnunua mtumwa wa kuhudumu msikitini, hilo ni jambo linalokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

[1] 03:35

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 234
  • Imechapishwa: 20/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´