Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) alijadiliana na watu wake juu ya kuabudu nyota. Aliona nyota, mwezi na jua. Wakati alipoona vinatoweka na kuondoka, hapo ndipo akabainisha ya kwamba haijuzu kuviabudu badala ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa kuwa vinafikiwa na kuja, kupotea, kugeuka na mengineyo. Hapo ndipo akawabainishia ubatili wa kuviabudu badala ya Allaah (´Azza wa Jall). Alifanya haya kwa ajili ya kutaka kujadiliana nao na sio kwa ajili ya kuviabudu kama wanavosema wanafalsafa. Alifanya haya kwa ajili ya kujadiliana nao na kuwabainishia upotevu wa kuabudu vitu hivi ambavyo vinaendeshwa na kupelekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kuvitoa katika kuchomoza na kuvipeleka katika kuzama na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1430-2-12.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015