Mzazi kumpenda mtoto wake kupitiliza

Swali: Mtu akimpenda mtoto wake mapenzi ya kimaumbile, lakini hata hivyo akawa amempenda kupitiliza mpaka akachelea asije kumpenda kama anavyompenda Allaah ni katika mambo ambayo anatakiwa kukatazwa?

Jibu: Ndio, akiyapa kipaumbele mapenzi ya mtoto mbele ya mapenzi ya Allaah basi itambulike kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا

“Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Mtume Wake na kufanya jihaad katika njia Yake, basi ngojeeni… “” (09:24)

Haya ni matishio ambapo Allaah anawaambia msubiri kitachowafika.

وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ

“… Allaah haongoi watu mafasiki.” (09:24)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa ni wapenzi ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imani.” (09:23)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136
  • Imechapishwa: 12/07/2020