Swali: Mama yangu – Allaah amjaze kheri – ni mwenye kuhifadhi swalah kwa wakati wake na anawapendea kheri wanawe na wenye kuhitajia. Mimi nampenda na namtamania kila kheri. Lakini hajui yanayosemwa kwenye Rukuu´, Sujuud na Tashahhud. Usomaji wake wa al-Faatihah ni wa kubadilisha maana. Wakati huohuo amehifadhi mashairi na hekima na anasema kuwa hajui na inatosheleza wanachuoni kusema:

“Asiyejua inatosheleza kwake kuleta Tasbiyh.”

Watoto wake hawana kipingamizi cha kumfundisha. Ninakuomba umhimize kwa hilo na kwa yale yatakayomnufaisha.

Jibu: Ikiwa anakubali kufunzwa na kustafidi na ni mwenye kufahamu anapofundishwa, basi ni wajibu kwenu kumfundisha. Haijuzu kwake kuswali isipokuwa mpaka baada ya kujifunza al-Faatihah. Angalau kwa uchache al-Faatihah ni wajibu. Swalah yake haisihi isipokuwa kwayo. Ama ikiwa hakubali kufunzwa kwa maana ya kwamba hafahamu anayofunzwa, hata akifunzwa hafahamu na haelewi, huyu aswali vile hali yake itavokuwa. Allaah (Ta´ala) Anasema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_01.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015