Mwenye kukaa I´tikaaf kuchaji simu kwa umeme wa msikiti

Swali: Je, inafaa kwa ambaye anafanya I´tikaaf kufaidika na umeme wa msikiti Mtakatifu katika kuchaji betri ya simu?

Jibu: Vitu vidogo havina neno. Kuchaji simu ni jambo dogo lisilodhuru umeme na halichukui moto mkubwa. Hili ni jambo linalosamehewa khaswa kwa anayekaa I´tikaaf ambaye hawezi kutoka. Hapana vibaya akachaji simu kwa umeme wa msikiti. Kwa sababu ni jambo lisilodhuru umeme.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=KN0Q4G7uwy8&t=33s
  • Imechapishwa: 18/01/2024